Je, unahangaika kupata mbinu za kubeti katika mpira wa miguu na umechoka kupoteza pesa kwa kampuni za kubeti?
Ikiwa ndivyo, sikiliza… Katika makala hii tutaangalia mbinu 5 za kubeti mpira wa miguu ambazo unaweza kutumia kushinda mikeka kila siku!
Mwongozo huu ndio dawa ya kubeti au tunaweza sema ndio uchawi wa kubeti kwani utakuonyesha kwa kina jinsi ya kuyashinda kila siku makapuni ya kubeti.
Tuanze!
Kubobea katika ligi au aina fulani ya mashindano ni moja ya mbinu bora ya kubeti kwani utakua na uelewa wa kina na uzoefu na mambo yanayotokea katika ligi au mashindano hayo. mfano unaweza kuamua kubobea katika ligi ya uingereza, ukaamua kufuatilia kwa undani fomu za timu, fomu za wachezaji, transfer na hata changamoto za kiufundi.
Ujuzi huu utakusaidia katika kubeti kwani utaweka mikeka inayotokana na facts sahihi, hivyo kupelekea kupata mikeka yenye uwezekano kushinda kila mara.
Ni muhimu kutambua kwamba kubobea katika mashindano au ligi fulani haimaanishi kujinyima katika ligi au mchezo mmoja tu, bali ni kuchagua maeneo machache ya kuzingatia na kukazia ili kuwa mtaalam katika maeneo hayo.
Ni mbinu ya kubeti inayohusisha kuchambua michezo na takwimu zilizopita ili kutabiri matokeo yajayo. Ndugu wanabeti ili kubeti na kufanikiwa wala hauhitaji uchawi au dawa! Mbinu sahihi ndio dawa ya kubeti na kushinda kila siku.
Tunapozungumzia hand capping tunamaanisha kuchambua mambo muhimu katika timu kama vile uchezaji wa timu, ubora wa wachezaji, rekodi za head to head, majeraha ya wachezaji na mengine mengi. Uchambuzi huu utatusaidia kufahamu ubora na udhaifu uko upande upi ili tuweze kutabiri matokeo yanayoweza kutokea katika mchezo.
Wadau wanaotumia mbinu hii huchanganua mienendo na kuisoma michezo iliyopita ili kubaini ni mambo gani yanaweza kutokea kisha kuweka beti katika mambo hayo. Mfano timu fulani ni imara katika safu ya ufungaji na timu B ni dhaifu katika defensi yao hivyo kuweka beti kwamba timu A itashinda.
Handcapping inaweza kuwa mbinu inayotumia muda mwingi lakini ni njia yenye faida kwa wale ambao wako tayari kuweka bidii kuuelewa mchezo na sababu zinazoathiri matokeo.
Ndiyo, value betting ni mbinu ya kubeti inayohusisha kutambua odds ambazo ni kubwa kuliko uwezekano halisi wa matokeo fulani kutokea.
Kwa maneno mengine mwana beti smart hutafuta mahali ambapo odds zilizowekwa na kampuni ya kubeti ni kubwa kuliko uwezekano wa tukio fulani kutokea.
Baada ya kutambua dau lenye thamani, tunaweza kuweka beti kwenye matokeo hayo tukitarajia faida nzuri kwenye uwekezaji wetu. Hii ni kwa sababu tunakuwa tumepata odds bora zenye thamani kuliko inavyopaswa. Kwa kufanya hivi kwa muda mrefu tuna uhakika wa kupata faida.
Value betting ni mbinu yenye faida kwa wale watakao weza kutambua odds zenye thamani kubwa zaidi na watakaoweza kuwa na nidhamu ya kufuata mbinu hii, kwani upata odds bora kuliko wanazotoa kampuni za kubeti hivyo kuwa katika upande faida.