Hesabu za mkeka ni hesabu rahisi na zisizoumiza kichwa. Kiasi unachoweza kushinda hupatikana kutokana na kuzidishwa kiasi ulicho beti (stake) pamoja na odds zote za mkeka wako.
Mfano umebeti kwenye mechi ya mpira kati ya Barcelona na Real Madrid. Kampuni ya kubeti hutoa odds kiotomatiki kwa kila tukio linaloweza kutokea katika mchezo mfano Barcelona kushinda, kutoa droo, idadi ya magoli itakayofungwa na kadhalika.
Ikiwa uliweka beti kwamba Barcelona itashinda, na odds za barcelona kushinda ni 2.3, kiwango chako cha kushinda ni 2.3 x (kiasi chochote ulichoweka kama dau kwenye mchezo huo).
Iwapo ubashiri wako utaenda sawa na uli weka dau kiasi cha Tsh10,000, ushindi wako ni 2.3 x Tsh 10,000 = Tsh 20,300.
Mfano huo ni kwa timu moja na dau moja. Kwa timu zaidi ya moja na dau zaidi ya moja, fomula ni hiyo hiyo isipokua utazidisha odds zote na kisha kuzidisha kwa dau uliloweka ili kupata ushindi wako.
Ikiwa ubashiri wako hautafaulu, utapoteza dau lako lote na kuishia kubaki na sifuri.